
Mchezaji wa Simba, Kibu Denis, akifunga bao timu ya Stellenbosch jana.
Na Mwandishi Wetu, Zanzibar
Timu ya Simba SC ni kama imetanguliza mguu kwenye Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuichapa Stellenbosch ya Afrika Kusini bao 1-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa jana Aprili 20, 2025 kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, visiwani Zanzibar.
Mechi ya marudiano ya nusu fainali ya mashindano hayo itachezwa Afrika Kusini Aprili 27, 2025 ambapo Stellenbosch itakuwa nyumbani, na mshindi wa matokeo ya jumla (aggregate) ya michezo yote miwili ataingia fainali kuchuana na mshindi kati ya RS Berkane ya Morocco na Constantine ya Algeria.

Wachezaji wa Simba wakishangilia ushindi
Simba waliupeleka mchezo huo visiwani Zanzibar baada ya Uwanja wa Taifa "kwa Mkapa" wa jijini Dar es Salaam ambao wamekuwa wakiutumia kwa michezo yao ya nyumbani kufungiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) mpaka pale utakapofanyiwa maboresho zaidi.
No comments:
Post a Comment