
Rais wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traore (kushoto) akisalimiana na Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete jijini Ouagadougou.
-----------------------------------
Na Mwandishi Wetu
Rais Mstaafu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amewasilisha ujumbe maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Rais wa Burkina Faso, Kapteni Ibrahim Traore.
“Rais Samia amenituma nije kuwasilisha ujumbe maalum kwako na nimefurahi umenipa fursa hiyo na umeupokea,” Dkt Kikwete alimwambia Rais Traore.

Rais Traore (kulia) akipokea ujumbe maalum wa Rais Samia kutoka kwa Dkt Kikwete.
----------------------------------
Pia, Dkt Kikwete aliwasilisha salamu za Rais Samia kuhusu umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya nchi za Afrika, hususan kubadilishana uzoefu, ili kwa pamoja bara hilo liweze kuendeleza rasilimali zake kwa faida ya watu wake.
Dkt Kikwete alifanya ziara Burkina Faso kama Mjumbe Maalum wa Rais Samia, ambapo alihudhuria mkutano maalum wa maafisa waandamizi kutoka serikali zote mbili - uliofanyika jijini Ouagadougou juzi Aprili 17, 2025.

Picha ya pamoja ya maafisa waandamizi kutoka serikali za Tanzania na Burkina Faso waliokutana jijini Ouagadougou juzi.
No comments:
Post a Comment