NEWS

Sunday, 4 May 2025

Mara: Hoteli ya kifahari ya CMG yazinduliwa kwa kishindo Tarime



Waziri wa Madini, Anthony Mavunde (katikati), akizindua ramsi Hoteli ya kifahari ya CMG mjini Tarime juzi. (Picha na Mara Online News)
----------------------------------------

Na Mwandishi Wetu, Tarime

Hoteli ya kifahari ya CMG imezinduliwa rasmi katika mji wa Tarime, mkoani Mara.

Uzinduzi wa hoteli hiyo ambao ni wa aina yake ulifanyika juzi Jumamosi na kushuhudia wageni mbalimbali, wakimeo viongozi na wananchi wa mkoa huo.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo alikuwa Waziri wa Madini, Anthony Mavunde.

Wakazi wa mji wa Tarime walipokea uzinduzi wa hoteli hiyo huku wakimpongeza Mkurugenzi wake, Christopher Mwita Gachuma, kwa kufanya uwekezaji huo mkubwa ambao utasaidia kupaisha sekta ya utalii katika mji wa Tarime na mkoa wa Mara kwa ujumla.

Hoteli hiyo inatarajiwa kuwa inapokea wageni wa ndani na nje ya nchi, wakiwemo watalii wanaotembelea Hifadhi ya Taifa Serengeti kupitia mpaka wa Sirari na uwanja mdogo wa ndege wa Magena uliopo nje kidogo ya mji wa Tarime.

Mwanamuziku maarufu nchini Tanzania, Diamond Platnumz alipata fursa ya kutumbuiza wageni walioshiriki katika uzinduzi huo.

“Tumeboresha sana vyumba vya kulala kwa viwango vya kimataifa. Ukiingia kwenye chumba cha hoteli ya kifahari kule Dubai ukafumba macho, kisha ukaja ukaingizwa kwenye chumba cha hapa CMG na kufumbua macho, utafikiri bado uko Dubai.

“Tumeboresha pia vyumba vya suti ambavyo kiongozi yeyote wa nchi, hata rais anaweza akakaa na wasaidizi wake,” anasema Mkurugenzi wa CMG Hotels Ltd, Christopher Mwita Gachuma.

Maboresho ya hoteli hiyo pia yamehusisha ujenzi wa ‘swimming pools’, vyumba vya sauna, mazoezi (gym) na huduma za massage.

“Pia, tumetenga maeneo maalum kwa ajili ya wageni kujenga mahema yao, kupiga picha na michezo ya watoto,” Gachuma aliliambia Gazeti maarufu la mkoa wa Mara la Sauti ya Mara hotelini hapo hivi karibuni.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages