![]() |
Muonekano wa sehemu ya Daraja la JP Magufuli “Kigongo |
----------------------------
NA MWANDISHI WETU, Mwanza
----------------------------------------------
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Daraja la JP Magufuli “Kigongo – Busisi” jijini Mwanza mwezi ujao.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alidokeza hilo wiki iliyopita wakati akikagua daraja hilo lenye urefu wa kilomita tatu na barabara zake unganishi zenye urefu wa kilomita 1.66.
Daraja hilo la juu ya maji katika Ziwa Victoria, limejengwa kwa fedha za ndani, na linatajwa kuwa ndilo refu zaidi katika Afrika Mashariki na Kati, na la tatu kwa urefu duniani.
Katika ziara hiyo, Waziri Mkuu Majaliwa aliambatana na Waziri wa Ujenzi, Abdallah Ulega, ambaye alitoa wito kwa wananchi wa wilaya za Misungwi, Sengerema na mkoa wa Mwanza kwa ujumla kujitokeza kwa wingi katika hafla ya uzinduzi wa daraja hilo la kihistoria.
Ujenzi wa daraja hilo uliasisiwa na kuanza kutekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais John Pombe Magufuli (kwa sasa ni marehemu), kisha kuendelezwa hadi kukamilishwa na Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Samia.
No comments:
Post a Comment