NEWS

Monday, 26 May 2025

RS Berkane ya Morocco yatwaa Kombe la Shirikisho Afrika 2025 dhidi ya Simba ya Tanzania



Mchezaji wa Simba SC, Shomari Kapombe (katikati), akijaribu kuwatoka wachezaji wa RS Berkane katika mechi ya fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwenye Uwanja wa New Amani, Zanzibar jana Jumapili.
------------------------------------------

Klabu ya Morocco - RS Berkane imetawazwa mabingwa wa Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa mara ya tatu baada ya sare ya 1-1 ugenini dhidi ya Simba SC ya Tanzania na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-1 katika fainali iliyochezwa jana Jumapili kwenye Uwanja wa New Amani, kisiwani Zanzibar, Tanzania.

Simba walijipa matumaini kwa bao la mapema la Joshua Mutale dakika ya 17, lakini kasi yao ilidhibitiwa baada ya beki Yusuf Kagoma kutolewa nje kwa kadi nyekundu dakika ya tano kipindi cha pili.

Licha ya Simba SC Simba kuonesha mchezo mzuri na ari ya kutaka kushinda, Berkane ilionesha mchezo wa kiwango cha juu zaidi.

Uwanja wa Amani ulijaa tafrani huku Simba wakifunga bao la pili baada ya Steven Mukwala kufunga kwa kichwa kizuri kilichompita kipa Munir Mohamed.

Hata hivyo, mashabiki hao walinyamazishwa dakika chache baadaye baada ya VAR kusema kwamba alikuwa ameotea.

Taji hilo linaashiria ushindi wa tatu wa RS Berkane wa Kombe la Shirikisho la CAF katika kipindi cha miaka mitano, na hivyo kuimarisha sifa yao kama moja ya vilabu vyenye msimamo thabiti katika misimu ya hivi karibuni.

Renaissance Berkane ilifanikiwa kufuzu kwa fainali ya Kombe la Shirikisho baada ya kuitoa timu ya Algeria, CS Constantine, katika nusu fainali kwa jumla ya mabao 4-1, huku Simba ikifuzu kupitia mikwaju ya penalti baada ya kutoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya klabu ya Al-Masry ya Misri.
Chanzo: BBC Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages