NEWS

Wednesday, 28 May 2025

Vijana waliohitimu kidato cha sita 2025 waitwa kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa



 
Jeshi la Kujenga Taifa JKT limewataka vijana waliohitimu kidato cha sita mwaka 2025 kutoka shule mbalimbali hapa nchini kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo kwa mujibu wa sheria ambapo wanatakiwa kuanza kuripoti kuanzia  Mei 28, hadi Juni 8 mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari Mei 27, 2025 Jijini Dodoma kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa JKT. Meja Jenerali Rajabu Mabele, Kaimu Mkuu wa Tawi la Utawala wa JKT, Kanali Juma Mray amezitaja baadhi ya kambi ambazo vijana hao wanatakiwa kuripoti huku wakiwa na vifaa vinavyohitajika.

Kanali Mray amefafanua zaidi ya kuwa kwa vijana wenye ulemavu wa kuona kwa macho wanapaswa kuripoti katika kambi ya Ruvu ilioko mkoani Pwani kwani ndio kambi yenye miondombinu ya kuwawezesha kupata mafunzo.

Kanali Mray amesisitiza kuwa nafasi hizo zinatolewa bure na zinapatikana katika tovuti ambayo imeainishwa na JKT huku akiwasisitiza wanafunzi waliohitimu kidato cha sita mwaka huu na jamii kwa ujumla wasikubali kurubuniwa kuhusu nafasi hizo.
 
Vifaa vinavyohitajika kuripoti navyo:
Kanali Mray ametaja baadhi ya vifaa ambavyo wanapaswa kuripoti navyo kuwa ni bukta ya rangi ya 'dark blue' yenye mpira kiunoni(plastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu, track suit ya rangi ya kijani au blue, nakala zote zinazohitajika katika udahili wa kujiunga na elimu ya juu, zikiwemo cheti cha kuzaliwa.
 
Namna ya kufahamu kambi uliyopangiwa:
Amesema ili kufahamu kambi ambayo kijana amepangiwa atatakiwa kuingiza jina la shule au namba ya shule aliyohitimu elimu ya kidato cha sita ndipo atapata orodha kamili ya majina hayo.
Chanzo:Muungwana
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages