NEWS

Tuesday, 13 May 2025

Rais Samia aongoza mazishi ya Waziri Mkuu Mstaafu Cleopa Msuya



 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Samia Suluhu Hassan, jana aliongoza mazishi ya Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais mstaafu, Mzee Ckeopa David Msuya, aliyefariki wiki iliyopita Mei 7, 2025.

Mazishi hayo, yaliyofanyika kijijini Usangi, pia yalihudhuriwa na viongozi wa ngazi za juu serikalini, wakiwemo wastaafu, pamoja na maelfu kwa maelfu ya wananchi wa wilaya ya Mwanga na mikoa ya jirani.

Kabla ya mazishi hayo ibada ya kumwombea marehemu ilifanyika katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Mchungaji Mwema, Usharika wa Usangi Kivindu, Dayosisi ya Mwanga, Jimbo la Kaskazini mkoani Kilimanjaro.

Hayati Mzee Msuya kwanza aliagwa na maelfu ya wananchi wa jiji la Dar es Salaam ambako alipatwa na umauti katika hospitali ya Mzena kabla ya mwili wake kusafirishwa kwenda wilayani Mwanga eneo alikozaliwa.

Mzee huyo, ambaye alifanya kazi bega kwa bega na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, baada ya uhuru, nyuma yake ameacha sifa za uchapaji kazi na uadilifu hadi wakazi wa wilaya ya Mwanga wakampa jina la heshima la Baba wa Mwanga kwa sababu ya kuwahamasisha wajiletee maendeleo kwa kuheshimu kazi.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages