
Nyambari Nyangwine (kushoto) akikabidhiwa fomu ya ubunge wa jimbo la Tarime Vijijini katika kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Hamza Kyeibanja.
----------------------------------------
Na Mwandishi Wetu, Tarime
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nyambari Nyangwine, kwa mara nyingine tena amechukua fomu ya kuomba ridhaa ya chama hicho tawala kugombea kiti cha ubunge jimbo la Tarime Vijijini katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu [2025].
Mwaka 2010 Nyambari alichaguliwa na wananchi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime - nafasi ambayo aliitumikia hadi mwaka 2015, na katika kipindi cha uongozi wake jimbo hilo liligawanywa kuwa majimbo mawili ya uchaguzi ambayo ni Tarime Vijijini na Tarime Mjini.
Mbali na kuwa mwanasiasa, Nyambari Nyangwine ni mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini.
No comments:
Post a Comment