
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, akimkabidhi Nyambari Nyangwine (aliyevaa kofia) tuzo ya pongezi na kumtambua kama mdau mashuhuri mwenye mchango wa kuimarisha elimu nchini, wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya TET jijini Dar es Salaam jana.
----------------------------------------
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
Mmoja wa wadau mashuhuri wa elimu nchini, Nyambari Nyangwine, jana alitoa shilingi milioni 110 kuichangia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Nyambari alitoa kiasi hicho cha fedha wakati wa Maadhimisho ya Miaka 50 ya TET yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.
Lengo la mchango huo ni kuunga mkono juhudi za TET katika kuboresha uwiano wa vitabu kwa wanafunzi kutoka kimoja kwa wanafunzi watatu hadi kimoja kwa kila mwanafunzi.
Katika hafla hiyo, Nyambari alitunukiwa tuzo kutokana na mchango wake wa kuimarisha sekta ya elimu nchini.
Nyambari alikabidhiwa tuzo hiyo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, katika maadhimisho hayo ya kutimiza nusu karne ya TET.
Mbali na kuwa mfanyabiashara, mwandishi na mchapishaji wa vitabu maarufu nchini, Nyambari ni mmoja wafanyabiashara wazawa ambao wameanza kuwekeza nje ya Tanzania, huku kampuni zake, yaani Nyambari Nyangiwine Group of Companies zikitajwa kufanya vizuri zaidi katika sekta ya kuchapisha vitabu.
Nyambari Nyangwine pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye amepata kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara mwaka 20210 hadi 2015.

Waziri Mkuu Majaliwa ambaye alimwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kama mgeni rasmi katika maadhimisho hayo, alisema serikali itaendelea kuimarisha TET ili kufikia maono yake ya kuwa kitovu cha ubora katika uandaaji, ukuzaji na ubunifu wa mitaala.
Alisisitiza kuwa TET ni moyo wa ukuaji wa elimu nchini kwa kuwa ndiyo inajenga msingi wa elimu kuanzia darasa la awali hadi kidato cha sita.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dkt. Aneth Komba, alisema katika kipindi cha miaka 50, serikali kupitia taasisi hiyo imefanikiwa kuongeza hazina ya vitabu vya kiada, ziada, riwaya, hadithi, ushairi na aina nyingie ya uandishi bunifu, moduli na maudhui ya kieletroniki yanayolenga kuwaongezea wanafunzi maarifa kwa kutathnimi vitabu vya ziada 1,146 vinavyoandikwa na wachapishaji binafsi.
Unaweza pia kusoma:
»Yametimia Mwanza: Rais Samia azindua Daraja la JP Magufuli “Kigongo Busisi” Ziwa Victoria
»Tarime Vijijini: Nyambari achangia milioni 5/- ujenzi Kanisa Katoliki Kitenga, aungwa mkono na madiwani 20 – zapatikana milioni 11/-
»Waitara azishukia kamati za siasa CCM Musoma Mjini na Tarime, atamani zifutwe
No comments:
Post a Comment