Dar es Salaam
Baraza la Mitihani Tanzania (Necta) limetangaza rasmi matokeo ya mtihani wa Kidato cha Sita wa mwaka 2025, uliofanyika kuanzia Mei 5 hadi 26, 2025.
Taarifa ilitolewa Jumatatu, Julai 7, 2025, visiwani Zanzibar, na kutangazwa na Katibu Mtendaji wa baraza la mtihani Tanzania Necta, Profesa Said Mohamed
Mtihani huu uliwashirikisha wanafunzi kutoka shule mbalimbali nchini, ambapo waliofaulu wanapata nafasi ya kusonga mbele kwa elimu ya juu (vyuo vikuu) au vyuo vya kati.
Kwa miaka ya karibuni Baraza la mtihani Tanzania (NECTA) lilifuta utaratibu wa kutangaza wanafunzi bora na shule bora zilizofanya vizuri.
Hili lilifanywa kwa maelezo kuwa baraza lilikuwa linataka kuleta usawa na kupunguza hali ya baadhi ya shule kuonekana ni bora kuliko shule nyingine
Hata hivyo wadau mbalimbali wa elimu walikosoa utaratibu huo wakisema, badala ya kufuta utaratibu huo, serikali ilitakiwa kuboresha shule za umma kwa kuwa karibu miaka yote, shule na wanafunzi waliokuwa wakifanya vizuri walikuwa kutoka shule binafsi na zile zinazomilikiwa na za taasisi hasa za dini.
No comments:
Post a Comment