
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, akizungumza katika mkutano maalum na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dodoma, Julai 18, 2025.
---------------------------------------
Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Kanali Evans Mtambi amewakaribisha waandishi wa habari nchini kutembelea mkoa huo ili kujionea vivutio mbalimbali vya utalii, ikiwemo hifadhi bora duniani – Hifadhi ya Taifa Serengeti.
Mbali na Hifadhi ya Serengeti, kiongozi huyo wa mkoa amewakaribisha kutembelea kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wilayani Butiama.
Kanali Mtambi alikuwa akitoa taarifa ya mafanikio ya Serikali ya Awamu ya Sita mkoani Mara, katika mkutano maalum na waandishi wa habari jijini Dodoma jana Ijumaa.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Alfred Mtambi, akizungumza katika mkutano huo.
---------------------------------------
“Ninawakaribisha sana mkoani Mara kutembelea kaburi la Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Hifadhi ya Taifa Serengeti, fukwe za Ziwa Victoria. Na sio hivyo tu, mje basi mkale nyama na kugonga kichuri,” Kanali Mtambi aliwambia waandishi wa wahabari, huku wakionekana kufurahia ukaribisho wa kiongozi huyo.
Alisema mkoa huo unafanya vizuri katika sekta ya ufugaji wa ng’ombe ambao nyama choma yake ni bora na tamu zaidi.
Kanali Mtambi amepata kukaririwa na vyombo vya habari siku za nyuma akisema “Hakuna sehemu niliyowahi kula nyama choma super kama Mara.”
Katika mkutano huo na waandishi wa habari, Kanali Mtambi alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akisema ameupa mkoa wa Mara kipaumbele cha pekee katika utekelezaji wa miradi mingi, ikiwemo ya kimkakati.
No comments:
Post a Comment