
CEO wa Mara Online, Mugini Jacob (aliyevaa tai nyeusi), akikabidhi zawadi ya kompyuta kwa walimu na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibumaye jana Septemba 4, 2025.
--------------------------------------
Afisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Mara Online, Mugini Jacob, ameipatia Shule ya Msingi Kibumaye zawadi ya Kompyuta na kuaahidi kusaidia upatikanaji wa mashine aina ya printa kwa ajili ya kuchapa mitihani ya wanafunzi.
Vifaa hivyo vinatarajiwa kusaidia kuchochea maendeleo ya kitaaluma katika shule hiyo kongwe iliyopo Halmashauri ya Mji wa Tarime, mkoani Mara.
CEO Mugini ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, alikabidhi zawadi hiyo wakati wa Mahafali ya Darasa la Saba ya Shule ya Msingi Kibumaye yaliyofanyika jana Septemba 4, 2025.

Mgeni rasmi CEO Mugini (katikati) akiteta jambo kwa furaha na Mwalimu Defilina.
---------------------------------------
"Kibumaye ni jina kubwa limetoa hadi maprofesa, wanafunzi nawapongeza sana mmevumilia mpaka leo, bila ninyi tusengekuwa hapa.
"Ili mfanikiwe katika safari yenu ya masomo mdumishe nidhamu - mheshimu wazazi na kila mtu mpaka vyuo vikuu, yote yanawezekana huu ni mwazo tu," alisema Mugini ambaye pia ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC).
Aidha, CEO Mugini aliahidi ‘kumshika mkono’ mmoja wa wanafunzi wanatokea mazingira magumu - atakayepata alama za juu kwenye masomo ya sayansi, likiwemo la hesabu.

CEO Mugini akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba cheti cha kuhitimu.
----------------------------------------
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kibumaye, Defilina Marco Sibani na wafanyakazi walimshukuru CEO Mugini kwa zawadi hiyo wakisema itachochea maendeleo ya taaluma katika shule hiyo Kongwe.
Kwa upande mwingine, wazazi na wadau wa mbalimbali wa elimu waliungana na mgeni rasmi kuchanga fedha taslimu kwa ajili ya kugharimia ukarabati wa miundombinu ya shule hiyo, ikiwa ni ishara ya mahusiano mema kati yao na uongozi wa shule hiyo.
No comments:
Post a Comment