
Na Christopher Gamaina, Tarime



Wananchi zaidi ya 80 wanawakilisha makundi rika kutoka wilaya ya Tarime kwenye mafunzo yanayoendeshwa na Shirika la HelpAge Tanzania kupambana na ukatili wa kijinsia kwa wanawake, mabinti na watu wenye ulemavu.
Wawezeshaji wakuu wa mafunzo hayo ya siku mbili - ambayo yameanza leo Septemba 5, 2025 mjini Tarime, ni Joseph Mbasha na Leonard Ndamgoba kutoka HelpAge Tanzania.

Mafunzo hayo yanaendeshwa chini ya Mradi wa Chaguo Langu Haki Yangu - unaotekelezwa na HelpAge Tanzania kwa ufadhili wa Serikali ya Finland kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu (UNFPA).
Kwa mujibu wa Mbasha, Helpage Tanzania inatekeleza mradi huo katika wilaya za Butiama na Tarime mkoani Mara, Kishapu na Kahama mkoani Shinyanga na Unguja na Pemba, visiwani Zanzibar.

Kupitia mafunzo hayo kwa makundi rika, washiriki wanapata fursa ya kutoa mawazo, kuendesha mijadala na kushirikisha wanaume na vijana wa kiume katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.
“Tunataka wanaume na vijana wa kiume wawe sehemu ya mapambano haya ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake, mabinti na watu wenye ulemavu,” amesisitiza Mbasha ambaye ni Meneja Programu, Haki, Sera na Ushirikiano wa Wadau wa Shirika la HelpAge Tanzania.

No comments:
Post a Comment