NEWS

Wednesday, 3 September 2025

Dkt. Nchimbi amuomba Mpina aachane na ACT, arudi nyumbani CCM



Dkt. Nchimbi na Luhaga Mpina

NA MWANDISHI WETU, Meatu

MGOMBEA Mwenza wa Urais wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi, amemuomba aliyekuwa Mbunge wa Kisesa katika wilaya ya Meatu mkoani Simiyu, Luhaga Mpina, kurejea kwenye chama hicho, na ameahidi kumpokea kwa mikono miwili.

Akizungumza katika mkutano wake wa kampeni jimboni Kisesa jana, Dkt. Nchimbi alisema Mpina hana budi kurudi nyumbani - CCM kwa kuwa bado ni sehemu ya familia hiyo ya kisiasa.

“Atakayempigia simu Mpina amwambie kaka yake mkubwa alipita hapa. Mwambieni hasiponipigia kura atakuwa amekosa adabu ya Kisukuma kabisa, maana nilipopita si aliwaambia kwamba mimi kaka yake. Mwambie kaka yako alipita hapa na anasubiri. Akirudi tena, anataka urudishe hiyo kadi ya chama chako kipya, urudi CCM na mimi nitapokea kadi ya Mpina mwenyewe, simtumi mtu yoyote,” alisema Dkt. Nchimbi.

Mpina, ambaye aliwahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Kisesa kwa tiketi ya CCM tangu mwaka 2005, alihama chama hicho baada ya jina lake kukatwa katika mchakato wa kura za maoni, na kujiunga na ACT – Wazalendo.

Siku chache baada ya kujiunga na ACT – Wazalendo mwanzoni mwa Agosti mwaka huu, Mpina aliteuliwa kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, ingawa baadaye aliwekewa pingamini na mmoja wa wanachama wa chama hicho.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages