
Katibu wa NEC ya CCM - Uchumi na Fedha, Joshua Mirumbe (kulia), akimnadi mgombea ubunge wa Rorya, Jafari Wambura Chege, katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye viwanya vya Nyamaguku jimboni humo jana Jumamosi.
Na Mwandishi Wetu, Rorya
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) - Uchumi na Fedha, Joshua Mirumbe, amewanadi kwa wananchi wa jimbo la Rorya, mkoani Mara wagombea wa urais, ubunge na udiwani kupitia chama hicho.
Mirumbe ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu (CC) ya CCM Taifa, alikuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho katika viwanja vya Nyamaguku jimbo hilo jana Jumamosi.
Alisema wana-Rorya wana kila sababu ya mkumchagua Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kutokana na kazi kubwa aliyoifanya ya kuwaletea maendeleo katika sekta ya maji, ikiwemo miradi ya maji Komuge, Shirati na Nyamagaro hadi Tarime unaogharimu shilingi bilioni 134.
Alitaa miradi mingine kuwa ni miundombinu ya barabara inayosimamiwa na TARURA na TANROADS, ikiwemo ujenzi wa barabara ya lami Kuruya-Utegi ambao upembuzi umeanza na barabara ya lami Utegi-Shirati.
Kwa upande wa elimu ya sekondari, alisema wilaya ya Rorya imepokea shilingi zaidi ya 600, huku kwenye afya vituo vitatu vya afya - Luo Imbo, Nyancha na Suba vimejengwa kwa gharama ya shilingi bilioni 1.2.
Mbali na mgombea urais wa CCM, Mirumbe pia aliwaombea kura mgombea ubunge wa Rorya, Jafari Wambura Chege na madiwani wote kupitia chama hicho kutoka kata 26 za jimbo hilo.
No comments:
Post a Comment