NEWS

Monday, 22 September 2025

Serikali yavuna shilingi bilioni 793 za mrabaha sekta ya madini

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya madini mjini Geita jana

Na Mwandishi Wetu

Serikali ilivuna mrabaha wa shilingi bilioni 793 kutoka makampuni ya Geita Gold Mine na Buckreef baada ya makampuni hayo kuzalisha kilo 76,530 za dhahabu zenye thamani ya shilingi trilioni 11.38 katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2025, ilielezwa jana.

Takwimu hizo zilitolewa kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Nane ya Teknolojia ya madini yanayofanyika mjini Geita.

Maonesho hayo yalifunguliwa jana mjini humo na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Ilielezwa kwenye maonesho hayo kwamba katika kipindi hicho cha miaka mitano wachimbaji wadogo wa Geita walizalisha kilo 22,000 za dhahabu zenye thamani ya shilingi trilioni 3.44 ambapo serikali ilipata mrabaha wa shilingi bilioni 235.5.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Yahya Samamba, alimweleza Waziri Mkuu kwamba Tanzania imepiga hatua kwa kuwa na viwanda vya kutengeneza zana mbalimbali za uchimbaji madini.

Alisema katika mwaka wa fedha 2024-2025 tani 62 za dhahabu zimezalishwa ikilinganishwa na tani 40-50 zilizokuwa zikizalishwa kila mwaka kwa miaka iliyotangulia.

Kwa kuzalisha tani 62 za dhahabu, alisema Tanzania imekuwa ni miongoni mwa nchi tano bora barani Afrika.

Akizungumza katika uzinduzi wa maonesho hayo, Waziri Mkuu alisema kwa hivi sasa sekta ya madini ni nguzo kubwa ya uchumi wa Tanzania.

Aliweka mkazo kwenye uwekezaji wa matumizi ya teknolojia ili kuongeza tija na kuwa daraja la mageuzi kuanzia utafiti, uchimbaji na usafishaji madini na Biashara ya madini hayo.

Alisema serikali imeimarisha mifumo ya ukusanyaji mpato na udhibiti wa biashara ya madini na matumizi ya mifumo ya kielektroniki.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages