
Esther Matiko
Na Mwandishi Wetu
Jina la Esther Matiko kwa sasa ni maarufu kwenye siasa za Tanzania. Mwanasiasa huyu amezidi kuwa maarufu mara baada ya kuhamia chama tawala - CCM.
Nyota yake imezidi kung’ara zaidi hivi karibuni baada ya kuteuliwa kupeperusha bendera ya CCM katika kinyang’anyiro cha ubunge jimbo la Tarime Mjini kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika nchini Oktoba 29, 2025.
“Esther sasa anaweza kufanya vizuri zaidi katika kuwaletea wakazi wa Tarime Mjini maendeleo. Akifanikiwa kuwa mbunge wa CCM, kazi yake itakuwa rahisi kuliko alivyokuwa CHADEMA,” anasema mmoja wa wachambuzi wa masuala ya saisa na uongozi nchini.
Mwaka 2010 Esther alianza safari yake ya kisiasa baada ya kubahatika kuwa Mbunge wa Viti Maalumu kupitia CHADEMA na baadaye mwaka 2015 alichaguliwa kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini kupitia chama hicho cha upinzani.
Mwaka 2020 aligombea nafasi hiyo bila mafanikio lakini akabahatika kutelutwa tena kuwa Mbunge wa Viti Maalum kwa mara ya pili kupita CHADEMA.
Hadi sasa, Esther pia ni Mbunge wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) ambalo Rais wake ni aliyekuwa Spika wa Bunge la Tanzania, Dkt. Tulia Ackson.
“Akiwa mbunge wa jimbo mwaka 2010, kuna miradi mingi ambayo Esther alianzisha, ukiwemo ujenzi wa soko jipya la kisasa mabalo limebadilisha mji wa Tarime kuwa moja ya miji yenye masoko bora ndani ya mkoa wa Mara, Tunatarjia mengi atakapokuwa mbunge wa CCM,” anasema Mwita Marwa Mwita, mmoja wa makada wa CCM wilayani Tarime.
Esther anajulikana kama mwanasiasa msomi na mpenda maendeleo, hasa katika sekta za elimu, maji, afya na michezo.

Mgombea Mwenza wa Urais, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, akimnadi Esther Matiko katika jimbo la Tarime mjini hivi karibuni.
Akiwa Mbunge wa Viti Maalum, Esther alianzisha Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) kwa ajili ya kusaidia maeneo ya kijamii, wakiwemo watu wenye mahitaji maalum katika wilaya ya Tarime
Tayari kupitia shirika hilo, Esther ametoa misaada katika shule mbalimbali na kwa makundi ya kijamii
“Esther ni mwanasiasa mpole na mwenye moyo wa kusaidia jamii, ndio maana unaona ameamua hadi kuanzisha Matiko Foundioan,” anasema Bhoke John, mkazi wa mjini Tarime.
No comments:
Post a Comment