NEWS

Tuesday, 9 September 2025

Wasira alivyowanadi wagombea wa CCM Mara



Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, akiwanadi wagombea ubunge; Dkt. Wilson Mahera (jimbo la Butiama) na Mgore Miraji Kigera (jimbo la Musoma Mjini) wiki iliyopita. Aliyekaa ni Mwenyekiti wa chama hicho mkoani Mara, Patrick Chandi Marwa.

NA MWANDISHI WETU, Musoma
---------------------------------------------

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, mwanasiasa mkongwe mwenye maneno ya kusisimua mioyo, Stephen Wasira, amezindua kampeni za ubunge jimbo la Musoma Mjini kuelekea Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika nchini Oktoba 29, 2025.

Uzinduzi huo ulifanyika wiki iliyopita, ambapo Wasira alitumia nafasi hiyo kumnadi kwa wananchi mgombea mpya wa ubunge wa CCM katika jimbo hilo, Mgore Miradi Kigera na wagombea ubunge wengine wa chama hicho mkoani Mara.

Pia, Wasira aliwaomba wana-Mara na Watanzania kwa ujumla kumchagua Mwenyekiti wa CCM Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, anayegombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema katika kipindi cha miaka minne ya uongozi wa Rais Samia, maendeleo makubwa ya kisekta yamefanyika, ikiwa ni pamoja na kuboresha huduma za kijamii - afya, maji, elimu na miundombinu ya barabara.

Wasira alisisitiza kuwa lengo la CCM ni kuendelea kushika dola ili kuwatumikia wananchi, na ndio maana kimeandaa ilani bora ya uchaguzi inayojibu mahitaji ya Watanzania.

Awali, akizungumza katika kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Butiama, Wasira alimnadi mgombea ubunge katika jimbo hilo, Dkt. Wilson Mahera.

Wagombea wengine wa CCM katika mkoa wa Mara na majimbo yao yakiwa kwenye mabano ni Prof. Sospeter Muhongo (Musoma Vijijini), Jafari Wambura Chege (Rorya), Esther Matiko (Tarime Mjini), Mwita Waitara (Tarime Vijijini), Mary Daniel Joseph (Serengeti), Boniphace Getere (Bunda Vijijini), Esther Bulaya (Bunda Mjini) na Kangi Lugola (Mwibara).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages