
Dkt. Samia Suluhu Hassan akijiandaa kuweka shada la maua kwenye Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika eneo la Mwitongo, Butiama mkoani Mara leo Oktoba 10, 2025. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Stephen Wasira, na wengine ni Katibu Mkuu wa chama hicho, Dkt. Asha-Rose Migiro, Madaraka Nyerere na Chifu Japhet Wanzagi.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Oktoba 10, 2025 amezuru Kaburi la Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika eneo la Mwitongo wilayani Butiama, mkoani Mara ambapo amefanya mazungumzo na familia yake na kushiriki dua ya kumuombea.






Dkt. Samia akiteta jambo na Madaraka Nyerere, mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
Dkt. Samia yuko mkoani Mara tangu jana Alhamisi katika ziara ya kampeni zake kuelekea Uchaguzi Mkuu unaopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025.
Alipowasili jana Alhamisi, alihutubia mikutano ya kampeni kwa nyakati tofauti katika miji ya Bunda na Musoma.
Leo Ijumaa, baada ya kuzuru Kaburi la Baba wa Taifa, amehutubia mkutano wa kampeni Butiama, na anahitimisha ziara hiyo katika wilaya ya Serengeti.
No comments:
Post a Comment