NEWS

Friday, 10 October 2025

Jackson Kangoye aliyetimkia ACT arejea CCM, Dkt. Samia, Wasira wamshukuru



Jackson Kangoye

Na Mwandishi Wetu
Musoma
--------------

Mwanasiasa kijana Jackson Kangoye amerejea CCM na kupokewa kwa furaha mbele ya Mwenyekiti wa chama hicho, Dkt. Samia Suluhu Hassan na wasaidizi wake.

Kangoye alitimkia ACT Wazalendo hivi karibuni baada ya kukosa uteuzi wa kugombea ubunge katika jimbo la Tarime Mjini, mkoani Mara.

Alitangaza kurudi CCM jana Alhamisi mjini Musoma kwenye mkutano wa kampeni za Dkt. Samia anayegombea urais kuelekea Uchaguzi Mkuu unaopangwa kufanyika Oktoba 29, 2025.

"Niliposikia [Kangoye] ameghafirika amehama, nilimwita nyumbani kwangu... nafurahi amesikia sauti yangu," Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Stephen Wasira, alisema.

Naye Dkt. Samia alimwambia Kangoye "Tunakushukuru sana, tunakupokea kurudi nyumbani."

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages