
Dhahabu
Na Mwandishi Wetu
Matumaini ya kukua kwa uchumi wa Tanzania yanazidi kuongezeka baada ya Ripoti ya Benki Kuu (BoT) ya Septemba 2025 kueleza kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la dunia.
Ripoti hiyo fupi ya BoT imebaini kwamba uuzaji wa dhahabu umeongezeka kwa asilimia 35.5 na kufikia dola za Marekani 4,322.
Pamoja na kupanda kwa bei ya dhahabu, pia mauzo ya bidhaa za kilimo kwa Septemba yaliongezeka hadi kufikia dola milioni 1,411 sawa na ongezeko la aslimia 28.3.
Mazao ya kilimo ambayo mauzo yake yamejumuishwa kwenye ripoti hiyo ya BoT ni korosho, tumbaku na kahawa.
Nao uuzaji wa bidhaa za huduma nje ya nchi umeongezeka kwa asilimia 14.8 kwa mwaka na kufikia dola milioni 16,894.4 mwishoni mwa Agosti, 2025, ripoti imeeleza.
No comments:
Post a Comment