NEWS

Thursday, 2 October 2025

Rais Samia atengua vigogo DART, UDART, ateua wapya



Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametengua na kuteua viongozi wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) na Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART).

Taarifa iliyotolewa leo Oktoba 2, 2025 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, imewataja viongozi hao kuwa ni Said Habibu Tunda ambnaye ameteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa DART, kuchukua nafasi ya Dkt. Athumani Kihamia ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Mwingine ni Pius Andrew Ng’ingo ambaye ameteuliwa kuwa Mkurugenzi MKuu wa UDART, kuchukua nafasi ya Waziri Kindamba ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

“Uteuzi huu unaanza mara moja,” imeeleza taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Sharifa Nyanga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages