NEWS

Monday, 10 November 2025

Heche, Lema, viongozi wengine wa CHADEMA waachiwa kwa dhamana Dar



Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA (Bara), John Heche.

Na Mwandishi Wetu
Dar es Salaam
-------------------

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Bara, John Heche na viongozi wengine kadhaa wa chama hicho wameachiwa na Jeshi la Polisi kwa dhama leo jioni ya Jumatatu Novemba 10, 2025.

Kwa mujibu wa wakili wao, Hekima Mwasipu, Heche ameachiwa kwa dhamana baada ya kushikiliwa na Jeshi la Polisi toka Oktoba 22, 2025 alipokamatwa katika viunga vya Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar es Salaam.

Heche ameachiwa pamoja na viongozi wengine wa chama hicho, akiwemo Naibu Katibu Mkuu (Bara), Amani Golugwa, Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani, Boniface Jacob na Mjumbe wa Kamati Kuu, Godbless Lema.

Viongozi wote hao wameachiwa katika Kituo cha Polisi cha Osterbay jijini Dar es Salaam, na imeelezwa kuwa wanatakiwa kuripoti kituoni hapo kesho Jumanne saa tano asubuhi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages