NEWS

Monday, 10 November 2025

Rais Samia amteua Dkt. Nyansaho na wengine watano kuwa wabunge



Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho

Na Mwandishi Wetu

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho na wengine watano kuwa wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 29, 2025.

Dkt. Nyansaho ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).

Wengine walioteuliwa na Rais Samia kuwa wabunge ni Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM, Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa, Dkt. Dorothy Gwajima, Abdullah Ali Mwinyi, Balozi Khamis Mussa Omar na Balozi Mahmoud Thabit Kombo.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu Chamwano, Dodoma jana na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, ilisema Rais amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Ibara ya 66(1)(e) ya Katiba ya Jamhuri Muungano ya Mwaka 1977.

Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inampa Rais mamlaka ya kuteua watu 10 kuingia kwenye Bunge la Muungano huo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages