
Tido Mhando
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewateua magwiji wawili wa fani ya uandishi wa habari kumsaidia katika ofisi yake.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt. Moses Kusiluka, waandishi hao waandamizi ni Tido Mhando ambaye atakuwa Mshauri wa Rais wa Habari na Mawasiliano.
Mwanahabari mwingine aliyeteuliwa ni Bakari Machumu ambaye atakuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu.

Bakari Machumu
Machumu anachukuwa nafasi ya Sharifa Nyanga ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Mhando ni mwanahabari mkongwe ambaye amefanya kazi katika vyombo mbalimbali vya habari ndani na nje ya Tanzania.
Wakati huo huo, Rais Samia amemteua Lazaro Nyalandu kuwa Balozi.
No comments:
Post a Comment