NEWS

Sunday, 23 November 2025

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane Dkt. Tutindaga atunukiwa Tuzo ya Ubunifu Mazao ya Utalii



Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga George, akionesha Tuzo yake ya Ubunifu wa Mazao ya Utalii.

Na Mwandishi Wetu

Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane jijini Mwanza, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga George, ametunikiwa Tuzo maalum ya kutambua na kuthamini uwezo wake katika kubuni na kuendeleza mazao mapya ya utalii.

Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga alitunukiwa tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam, Novemba 20, 2005.

Tuzo hiyo inajulikana kama ‘Chief Innovation/Head of Product Design and Innovation of the Year katika Top 100 Executives List Awards 2025’.

Baadhi ya mazao ambayo Dkt. Tutindaga ameyabuni na kuyaendeleza katika HIfadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane ni Boat Safari katika Ziwa Victoria, rock hiking, uimarishaji wamMaeneo ya mapumziko (picnic sites), michezo majini, kutazama machweo ya jua na uboreshaji wa huduma za malazi ya kitalii.


Mkuu wa Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane, Kamishna Msadizi wa Uhifadhi Dkt. Tutindaga George, akipokea Tuzo ya Ubunifu wa Mazao ya Utalii, jijini Dar es Salaam.

“Nashukuru sana kupata nafasi na kama Mhifadhi naendelea kuwakaribisha kutembelea Hifadhi ya Taifa Kisiwa cha Saanane,” Dkt. Tutindaga aliuambia umati uliokuwa katika hafla hiyo.

Pia, alimshukuru Kamshina wa Uhifadhi (CC) wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Musa Kuji, kwa kutoa fursa kwa viongozi wanawake kuwa wabunifu kwa maendeleo ya uifadhi na utalii nchini.

“Tuzo hii ni pongezi kwa uongozi mzima wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania, namzunguiza Kamshina wa Uhifadhi Tanzania ambaye ametoa fursa kwetu sisi hususan viongozi wa kike, tumepata fursa ya kutekeleza majukumu yetu katika hali ambayo tunaweza kufanya ubunifu katika angles zote na hii leo imepelekea nipate tuzo hii,” alisema Dkt. Tutindaga.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages