NEWS

Tuesday, 11 November 2025

Zungu aibuka mshindi Uspika wa Bunge la Tanzania



Mussa Azzan Zungu

Na Mwandishi Wetu
Dodoma
-------------

Hatimaye Mbunge wa Ilala mkoani Dar es Salaam kupitia CCM, Mussa Azzan Zungu, ndiye Spika mpya wa Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Katika uchaguzi uliofanyika kwenye kikao cha kwanza cha mkutano wa kwanza wa bunge hilo jijini Dodoma leo Jumanne, Zungu amepata kura 378 kati ya 383 zilizopigwa na wabunge.

Kwa ushindi huo, Zungu anakuwa Spika wa Nane wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tangu kuanzishwa kwake, baada ya kuwashinda wagombea wa vyama vingine vya siasa waliopata jumla ya kura mbili.

Zungu aliteuliwa na chama chake - CCM kuwania nafasi hiyo, huku Spika aliyepita, Dkt. Tulia Ackson, akijitoa katika kinyang’anyiro hicho kwa sababu ambazo hazikuelezwa wazi.

Zungu ambaye alikuwa Naibu Spika wa Bunge la 12, naye sasa atasaidiwa na Daniel Sillo ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Spika wa Bunge 13.

Miongoni mwa waliowahi kushika wadhifa huo wa Spika katika historia ya Tanzania ni Adam Sapi Mkwawa, Erasto Andrew Mbwana Mang’enya, Pius Msekwa, Samuel John Sitta, Anna Makinda, Job Ndugai na Dkt. Tulia Ackson.
Read Also Section Example

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages