NEWS

Friday, 28 November 2025

Waziri Kijaji asema Tanzania ina uwezo wa kuongoza utalii barani Afrika



Na Mwandishi Wetu, Arusha
Tanzania ina uwezo mkubwa wa kushika nafasi ya kwanza ya utalii barani Afrika iwapo raslimali zake zilizopo zitalindwa na kutunzwa kwa umakini.

Hayo ni maoni ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt Ashatu Kijaji, alipotembelea jana Novemba 27, 2025 makao makuu ya Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) jijini Arusha.

Alisema, katika ziara hiyo ya kwanza tangu ashike wadhifa huo, kwamba kuwepo kwa uhifadhi wa raslimali za kuvutia watalii wengi nchini ni msingi wa uhai kwa uchumi wa Tanzania na fahari kwa taifa.

"Tuna misingi yote ya kuwa namba moja Afrika na duniani iwapo tu kutakuwepo ulinzi madhubuti wa raslimali zetu kwa kuwashirikisha wananchi," alisema.

Aliwataka wafanyakazi katika hifadhi za taifa kutoa huduma bora kwa wageni ambao wanaliingizia taifa fedha nyingi za kigeni.

Dkt Kijají alisema azma ya serikali ni kufikia watalii milioni nane ifikapo mwaka 2030, suala ambalo linazifanya taasisi chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii ili kufikia lengo hilo.

Kamishina wa Uhifadhi, Mussa Nassoro Kuji, alimwambia Waziri kwamba shirika lake litalinda bioanuai, kuboresha mifumo ya ulinzi wa wanyamapori na kusimamia raslimali za hifadhi kwa kutumia teknolojia na mbinu za kisasa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages