
Na Mwandishi Wetu


Hifadhi ya Taifa Serengeti imetangazwa kuwa Hifadhi Bora ya Taifa Duniani 2025 kwa mara nyingine tena na kuiweka Tanzania katika nafasi ya kuendelea kuvutia watatii wengi zaidi.
Tuzo ya ushindi wa hifadhi hiyo ilipokewa na Kamishna wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Musa Kuji, katika hafla ya utoaji wa Tuzo za Utalii Duniani 2025 (WTA 2025) zilizofanyika nchini Bahrain, Desemba 6, mwaka huu.

Hifadhi ya Taifa Serengeti ni moja ya kivutio kikubwa cha watalii wengi kutoka maeneo mbalimbali duniani, kutokana na misafara ya nyumbu wanaohama na wanyamapori wakubwa watano (Big Five), miongoni mwa wengine wengi.
Tuzo za WTA, ambazo mara nyingi huitwa Oscars za Utalii Duniani kutokana na hadhi yake kubwa, ziliwakutanisha washiriki zaidi ya 500, wakiwemo viongozi wa serikali na wadau wa sekta ya utalii.

Katika tuzo hizo, Tanzania imeshinda jumla ya tuzo nne, ikiwemo ile iliyoenda Zanzibar, ambayo imetajwa kama eneo bora Afrika kwa mikutano na matukio ya kitaasisi.
Pia, Tanzania imepata tuzo mbili katika kundi la sekta binafsi – ambazo ni kampuni bora ya Safari za Puto Duniani iliyochukuliwa na kampuni ya Serengeti Balloon Safaris na Jumaira Thanda Resort katika Kisiwa cha Mafia ambacho kimetangazwa kuwa kisiwa bora cha mapumziko duniani.
No comments:
Post a Comment