NEWS

Tuesday, 9 December 2025

Makuruma ampongeza Dkt. Madeni kwa kuinua mapato ya Halmashauri Serengeti



Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Mwita Makuruma (katikati), akimpongeza Mkurugenzi Dkt. Maulid Suleiman Madeni.

Na Mwandishi Wetu
Serengeti
-------------

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Mwita Makuruma, amempongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Dkt. Maulid Suleiman Madeni na timu yake ya wataalamu kwa juhudi kubwa wanazofanya kuinua ukusanyaji wa mapato ya ndani ya halmashauri hiyo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Mkutano wa Baraza la Tisa la Madiwani wa halmashauri hiyo, mjini Mugumu, Desemba 3, 2025, Makuruma alisema juhudi za Dkt. Madeni na timu yake ya wataalamu zimewezesha mapato ya ndani kuongezeka hadi shilingi bilioni 6.6 kwa mwaka.


Madiwani wakifuatilia hotuba ya Mwenyekiti Makuruma kikaoni

“Tuna timu mahiri ambayo inaongozwa na Dkt. Madeni, wakati anakuja [Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti] kimapato tulikuwa nyuma sana, lakini sasa tunaongoza kimkoa, ningependa kuendelea kufanya naye kazi,” alisisitiza Makuruma ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Busawe.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages