NEWS

Tuesday, 9 December 2025

Waziri Nyansaho azuru makao makuu ya Jeshi la Kujenga Taifa



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, akipanda mti wa kumbukumbu makao makuu ya JKT, jijini Dodoma.

Na Mwandishi Wetu
Dodoma
------------

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la kujenga Taifa (JKT), Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, Jumatatu Desemba 8, 2025, alifanya ziara ya kikazi kwa kutembelea makao makuu ya JKT, chamwino jijini Dodoma.

Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara zake za kikazi alizozianza kwa ajili ya kujitambulisha na kuzungumza na maafisa, askari na watumishi wa umma wa wizara hiyo.
Mara baada ya kuwasili, Waziri Nyansaho alipokewa na mwenyeji wake, Mkuu wa JKT, Meja Jenerali Rajabu Mabele na uongozi mzima wa jeshi hilo.

Pamoja na mambo mengine, waziri huyo alipata wasaa wa kupanda mti wa kumbukumbu na baadaye kuzungumza na maafisa, askari na watumishi wengine.

Katika hotuba yake, Waziri Dkt. Nyansaho alimpongeza Meja Jenerali Mabele kwa mapokezi mazuri, na kusema serikali kupitia wizara hiyo itaendelea kuiwezesha JKT ili itekeleze ipasavyo majukumu yake ya msingi ambayo ni malezi ya vijana, uzalishaji mali na ulinzi wa Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages