NEWS

Wednesday, 3 December 2025

Rais Samia ateta na Kiongozi wa Biashara Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na kuzungumza na Naibu Mwenyekiti wa Biashara ya Jumuiya ya Madola na Baraza la Uwekezaji (CWEIC), Lord Hugo Swire, Ikulu jijini Dar es Salaam, Jumanne Desemba 2, 2025.

Rais Samia na Naibu Mwenyekiti wa CWEIC Swire ambaye pia alikuwa Waziri wa zamani Mambo ya Nje wa ofisi ya Jumuiya ya Madola katika Serikali ya Uingereza, walijadiliana masuala ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara na uwekezaji ambao utachochea ukuaji wa uchumi na kutengeneza ajira.

Aidha, Lord Swire aliiomba Tanzania kuwa mshirika wa kimkakati ili kuchochea wawekezaji wengi kutoka washirika wa Jumuiya hiyo ya Madola.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages