NEWS

Tuesday, 9 December 2025

Tanzania, Marekani kuimarisha zaidi ushirikiano




Na Mwandishi Wetu
Dodoma
------------

Rais Samia Suluhu Hassan, Jumatatu Desemba 8, 2025, alifanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Andrew Lentz, kuhusu uimarishaji ushirikiano katika maeneo mbalimbali ya baina ya nchi hizo mbili.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Chamwino, Dodoma, ilieleza kuwa Balozi Lentz alimweleza Rais Samia azma ya nchi yake ya kukuza zaidi uhusiano wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama baina ya Tanzania na Marekani.

Mazungumzo hayo ya nchi hizo mbili pia yalijikita katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekekezwa na kampuni za Marekani hapa nchini.

Miradi ya kimkakati iliyogusiwa kwenye mazungumzo hayo ni pamoja na ule wa gesi silia na wa Tembo Nickel.

Ushirikiano wa Tanzania na Marekani katika sekta mbalimbali za kijamii na kiuchumi ulianza tangu Tanzania Bara ilipopata uhuru wake mwaka 1961.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages