
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa ngazi za juu wa JWTZ jijini Dodoma, jana Ijumaa.
Dodoma
------------
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amesema yuko tayari kutoa fikra mpya kuhusu malengo yanayokusudiwa ili Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liweze kutimiza majukumu yake.
Amesema serikali itafanya kila jitihada kuhakikisha kwamba jeshi hilo linatimiza majukumu yake kama ipasavyo.
Dkt Nyansaho aliyasema hayo alipotembelea Makao Makuu ya JWTZ eneo la Msalato jijini Dodoma, jana Ijumaa, kwa ajili ya kujitambulisha kwa maafisa wa ngazi za juu, askari na watumishi wengine wa makao makuu ya jeshi hilo.
Hiyo ilikuwa ziara yake ya kwanza baada ya kuteuliwa kuongoza wizara hiyo mwezi uliopita kufuatia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
No comments:
Post a Comment