NEWS

Thursday, 18 December 2025

Zifahamu familia 5 tajiri zaidi duniani na siri ya mafanikio



Chombo cha habari cha Marekani, Bloomberg, kimetoa orodha ya familia 25 tajiri zaidi duniani kwa mwaka 2025.

Wakati huo huo, familia ya kifalme ya Saudi Arabia (House of Saud) imepata ongezeko kubwa la utajiri wake mwaka huu, na sasa imeshika nafasi ya tatu kwenye orodha ya Bloomberg, ikilinganishwa na nafasi ya sita liyokuwa nayo mwaka jana.

Cha kuvutia zaidi, familia tatu kati ya tano tajiri zaidi duniani zinatoka katika ulimwengu wa Kiarabu.

Pia, familia ya Ambani kutoka India imeshika nafasi ya nane kwenye orodha hiyo ambayo inajumuisha familia nyingine nyingi, lakini katika makala hii, tunaangalia familia 5 za kwanza, utajiri wao na siri ya mafanikio yao.

5. Familia ya Egmez

Kampuni: Egmez

Jumla ya mali: Dola bilioni 184

Egmez ni miongoni mwa kampuni kubwa zaidi duniani za nguo na mitindo. Kwa sasa, takribani wanafamilia 100 wa kizazi cha sita cha familia ya Egmez wanaendesha biashara hiyo.

Mkurugenzi Mtendaji (CEO) wa kampuni hiyo ni Axel Domus

4. Familia ya Al Thani

Biashara: Mafuta, viwanda

Jumla ya mali: Dola bilioni 199

Maslahi ya familia tawala ya Al Thani nchini Qatar yanahusishwa moja kwa moja na biashara ya mafuta na gesi.

Takribani wanafamilia wote wanashikilia nyadhifa za juu serikalini na kudhibiti sekta mbalimbali za kiuchumi. Familia ni kubwa sana, lakini matawi machache ndiyo yanayoongoza utawala wa nchi.

3. Familia ya Kifalme ya Saudi Arabia

Biashara: Mafuta, viwanda

Jumla ya mali: Dola bilioni 213

Utajiri wa familia ya kifalme ya Saudi Arabia umeongezeka kwa kiwango kikubwa mwaka huu. Kwa mujibu wa orodha ya Bloomberg ya mwaka jana, familia hiyo ilikuwa na utajiri wa dola bilioni 140, lakini mwaka huu umeongezeka kwa dola bilioni 73.

Utajiri huu kwa kiasi kikubwa unatokana na biashara ya mafuta. Bloomberg ilikadiria mali ya familia hiyo kwa kuzingatia malipo yaliyofanywa kwa wanachama wa familia kutoka hazina ya kifalme kwa kipindi cha miaka 50.

Mali za ufalme zenye thamani ya dola zaidi ya bilioni 1 ziko chini ya usimamizi wa moja kwa moja wa Mwana mfalme Mohammed bin Salman.

2. Familia ya Al Nahyan

Chanzo kikuu cha utajiri wa familia ya Al Nahyan, familia tawala ya Falme za Kiarabu (UAE), ni biashara ya mafuta.

Mtawala wa Abu Dhabi, Sheikh Mohammed bin Zayed Al Nahyan, pia ni Rais wa Umoja wa Falme za Kiarabu.

1. Familia ya Walton

Familia ya Walton inamiliki takribani asilimia 44 ya hisa za maduka ya Walmart, na mtandao huo wa maduka makubwa ndiyo chanzo kikuu cha utajiri wao.

Walmart ina maduka 10,750 duniani kote na inahudumia takribani wateja milioni 270 kila wiki. Mwanzilishi wa Walmart, Sam Walton, aligawa mali yake kwa hekima miongoni mwa watoto wake wote ili kuimarisha umoja na nguvu ya biashara ya familia.

Kwa mujibu wa Bloomberg, sababu kuu ya ukuaji wa Walmart ni kulinda mali zake na kufanya mikataba ya biashara bila kupunguza umiliki wa familia.

Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages