
Waziri Dkt. Rhimo Nyansaho
Musoma
-------------
Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Mara, leo Jumanne, Januari 6, 2026 kimemchagua Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, kuwa Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo.
Awali, Mwenyekiti wa kikao hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi, amewasilisha jina la Dkt. Nyansaho, na wajumbe kwa kauli moja wakaridhia.
Kikao hicho kinachofanyika mjini Musoma, kinapokea taarifa za utekelezaji wa matengenezo ya barabara kuanzia Aprili hadi Septemba, 2025.
No comments:
Post a Comment