
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika picha ya pamoja na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji (kushoto) na Naibu Waziri, Hamad Chande, baada ya kukabidhiwa Tuzo za Utalii Duniani.
Zanzibar
-------------
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekabidhiwa rasmi Tuzo za Utalii Duniani.
Uongozi wa Wizara ya Maliasisli na utalii ulimkabidhi Rais Samia tuzo hizo, Jumatatu, Januari 5, 2026 katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, visiwani Zanzibar.
Ujumbe wa Wizara uliomkabidhi Rais Samia tuzo hizo uliongozwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Ashatu Kijaji.

Rais Samia akipokea tuzo kutoka kwa Waziri Kijaji
Rais Samia alikabidhiwa tuzo tatu ambazo ni “World’s Leading Safari Destination” - Tanzania, “World’s Leading National Park” - Hifadhi ya Taifa Serengeti na “Africa’s Leading Safari Destination” - Tanzania.
Tuzo hizo zilipatikana kufuatia ushindi wa Tanzania katika tuzo za utalii za kimataifa zilizotolewa na Shirika la World Travel Awards (WTA).

Tuzo alizokabidhiwa Rais Samia
Ushindi huo unaotokana na jitihada za Serikali ya Tanzania katika kukuza, kutangaza na kuendeleza sekta ya utalii kwa kiwango cha kimataifa.
Hafla ya kukabidhi tuzo hizo ilijumuisha viongozi mbalimbali, akiwemo Naibu Waziri wa Malisili na Utalii, Hamad Chande, Katibu Mkuu Wizara ya Malisili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi na Mkurugenzi wa Wanyamapori Tanzania, Dkt. Alexander Lobora.
Mkurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB), Ephraim Mafuru, Mkurugenzi wa Utalii Tanzania, Dkt. Thereza Mugobi na Kamishna wa Uhifadhi Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), CPA Musa Nassoro Kuji, miongoni mwa wengine.

No comments:
Post a Comment