NEWS

Thursday, 8 January 2026

Katambi, Makonda wapanda Baraza la Mawaziri



Patrobas Katambi na Paul Makonda

Na Mwandishi Wetu

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amemteua Patrobas Katambi kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, akichukua nafasi ya George Simbachawene ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Kabla ya uteuzi huo, Katambi alikuwa Naibu Waziri wa Viiwanda na Biashara.

Taarifa ya Ikulu Chamwino, Dodoma, iliyotolewa Januari 8, 2026 ilieleza pia kwamba Rais Samia amemteua Paul Makonda kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Makonda anachukua nafasi ya Profesa Palamagamba Kabudi ambaye ameteuliwa na Rais Samia kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Ikulu (Kazi Maalum).

Aidha, Rais Samia pia amemhamisha aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dennis Londo, kuwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara.

Naye Ayoub Mohamed ameteuliwa na Rais Samia kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages