NEWS

Tuesday, 20 January 2026

Mwasisi wa CHADEMA Edwin Mtei, afariki dunia

Mzee Edwin Mtei enzi za uhai wake
Na Mwandishi Wetu


Mwasisi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Gavana wa Kwanza wa Benki Kuu ya Tanzania ilipoanzishwa mwaka 1966, Edwin Mtei, amefariki dunia.


Mzee huyo, maarufu katika siasa za Tanzania baada ya uhuru, alifariki jijini Arusha jana Januari 19, 2026, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA, John Heche.


Mtei, 93, aliyezaliwa mkoani Kilimanjaro, aliitumikia Tanzania katika nyadhifa mbalimbali, ikiweno nafasi ya Waziri wa Fedha wakati wa uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere (1922-1999)


Huu ni msiba mkubwa si kwa CHADEMA tu bali kwa taifa zima la Tanzania ambalo limempoteza bingwa wa uchumi aliyeonyesha mwelekeo wa taifa katika zama za siasa za Ujamaa na Kujitegemea.


Wakati huo huo, Rais Samia Suluhu Hassan, ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha Mzee Mtei ambaye amesema alikuwa kielelezo cha utumishi uliotukuka nchini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages