
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya (katikati mbele), akikagua jengo la iliyokuwa Hoteli ya Kitalii ya Musoma, juzi.
akiripoti kutoka
Musoma
-------------


Musoma
-------------
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Dkt. Pius Stephen Chaya, amesema serikali imeanza mchakato wa kuleta wawekezaji kwa ajili ya kufufua viwanda vilivyotekelezwa kwa muda mrefu mkoani Mara.
Dkt. Chaya aliyasema hayo mjini Musoma juzi alipotembelea viwanda hivyo, kikwemo Kiwanda cha Nguo Musoma (MUTEX), Kiwanda cha Maziwa cha Musoma na Hoteli ya Kitalii ya Musoma.
"Kimsingi hivi ni viwanda vya zamani sana, kama tunataka kuvifufua tunaenda kuwekeza kwenye teknolojia. Tupo kwenye mkakati wa kutafuta wawekezaji wenye 'commitment', hatutaki kurudi kule tulikokuwa, watu walikuwa wakipewa viwanda na kubadilisha matumizi,” alisema.
Alisisitiza kuwa serikali imedhamiria kuwekeza kwenye viwanda ili kuchochea uchumi na ajira kwa vijana nchini na kwamba ili kuwa na kongani za viwanda lazima kila halmashauri iwe na ukanda wa kiuchumi.

Sehemu ya mbele ya jengo la Kiwanda cha Maziwa Musoma kilichotelekezwa
"Nimeona kiwanda cha maziwa, tunaendelea na mazungumzo na mwekezaji tutampa atoe 'commitment' kwamba ni lini anaanza kazi,” alisema na kuendelea:
"Musoma Hotel ni ya miaka ya 70’, tunakuja kusogeza SGR mpaka Musoma pamoja na miundombinu mingine. Nimuagize Msajili wa Hazina waharakishe kumpata mwekezaji na ujenzi uanze June.”
Naibu Waziri Chaya ambaye anatarajiwa kuhitimisha ziara yake ya siku tatu mkoani Mara leo, alitumia nafasi hiyo pia kuelekeza kila halmashauri nchini kutenga maeneo kwa ajili ya shughuli za kiuchumi za vijana.

Naibu Waziri Chaya akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mjini Musoma, Mara juzi. (Picha zote na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment