
Baba Mtakatifu, Papa Leo wa XIV, jana Jumatano, Januari 28, 2026 alipokea ujumbe wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt .Samia Suluhu Hassan, uliowasilishwa kwake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Thabit Kombo.
Waziri Kombo aliambatana na Waziri katika Ofisi ya Rais (Kazi Maalum), Prof. Palamagamba Kabudi na maofisa wa Ubalozi wa Tanzania huko Vatican.
Maudhui ya ujumbe uliowasilishwa kwa Papa Leo XIV hayakufafanuliwa lakini inaaminika yanalenga katika kukuza uhusiano wa miongo mingi kati ya Tanzania na Vatican.
No comments:
Post a Comment