NEWS

Tuesday, 27 January 2026

Rais Samia asherehekea ‘birthday’ yake kwa kupanda miti



Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akipanda mti wa muembe aina ya mangifera indica katika eneo la Bungi Kilimo, mkoani Kusini Unguja, ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku yake ya kuzaliwa - leo Januari 27, 2026.

Na Mwandishi Wetu
Zanzibar
----------------

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Januari 27, 2026 amesherehekea siku yake ya kuzaliwa (birthday) kwa kupanda miti katika eneo la Bungi Kilimo, mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.
“Shukrani kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu na mwingi wa rehema kwa kunijalia kuifikia siku nyingine ya kumbukizi ya kuzaliwa na umri wa miaka 66. Kwa moyo wa dhati, nimepokea na ninawashukuru nyote kwa salamu zenu za upendo.

“Nimesherehekea siku hii kwa kupanda miti. Wito wangu kwenu, tujenge na tuendeleze utamaduni wa kupanda miti na kutunza mazingira ili nayo yaendelee kututunza sisi na vizazi vijavyo,” Rais Samia ameandika kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii.

Rais Samia akikata keki kusherehekea kumbukizi ya 'birthday' yake leo

Samia alizaliwa Januari 27, 1960 katika kijiji cha Kizimkazi, mkoa wa Kusini Unguja, Zanzibar.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages