
Sehemu ya madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti wakiwa kikaoni hivi karibuni
Serengeti
----------------
Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti limepitisha rasmi mabadiliko ya jina la Mji wa Mugumu ambao sasa utajulikana kama Mamlaka ya Mji Mdogo wa Serengeti, kufuatia uamuzi huo ulioridhiwa katika kikao cha Baraza kilichofanyika Februari 17, 2026.
Akiwasilisha taarifa hiyo katika kikao cha Baraza hilo kilichofanyika Serengeti Februari 17, 2026, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ayub Mwita Makuruma, alisema mabadiliko hayo yamefanyika kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Namba 796, linalohusu Amri ya Mgawanyo wa Maeneo ya Utawala katika Serikali za Mitaa.

Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Ayub Mwita Makuruma (kulia), akiongoza kikao cha Baraza la Madiwani.
Makuruma alieleza kuwa hatua hiyo inalenga kuimarisha hadhi ya kiutawala ya eneo hilo sambamba na kuchochea kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika wilaya ya Serengeti.
No comments:
Post a Comment