NEWS

Wednesday, 4 February 2026

Mara: Wanne wanaswa kwa tuhuma za kuiba gari la wagonjwa na kulibadili kuwa la kubeba watalii Arusha



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, akionesha gari la wagonjwa lililoibwa jinsi lilivyobadilishwa rangi na muonekano.

Na Mwandishi Wetu
Musoma
----------------

Watu wanne wakiwamo watumishi wa serikali wanashikiliwa na Polisi mkoani Mara kwa tuhuma za kuiba gari la wagonjwa (ambulance).

Gari hilo, mali ya Halmashauri ya Manispaa ya Musoma - Mara, inaelezwa liliibwa Oktoba 25, 2025 usiku likiwa limeegeshwa nje ya ofisi ya Mkurugenzi wa manispaa hiyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Pius Lutumo, amewataja watuhumiwa wa wizi huo kuwa ni mkazi wa mjini Tarime, Goodluck Chacha (26).

Wengine na makazi yao yakiwa kwenye mabano ni Karume Kimwel - miaka 26 (Morombo mkoani Arusha), Said Ramadhani - 39 (Engosengyu - Arusha) na Elias Lyimo - 59 (jijini Arusha).

Taarifa ya RPC Lutumo kwa vyombo vya habari leo Jumatano imesema gari hilo la wagonjwa lilipatikana jijini Arusha likiwa katika hatua za mwisho kubadilishwa kuwa la kubeba watalii.


Gari hilo kabla ya kuibwa na kubadilishwa rangi na muonekano

Kamanda Lutumo amesema upelelezi umekamilika, hivyo watuhumiwa wa wizi wa ambulance hiyo wanatarajiwa kufikishwa mahakamani wakati wowote kujibu mashtaka yanayowakabili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages