NEWS

Friday, 13 March 2026

Chandi alipongeza Gazeti la Sauti ya Mara kwa kuzipa kipaumbele habari za maendeleo



Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa (kulia), akipokea nakala ya Gazeti la Sauri ya Mara kutoka kwa CEO na Mhariri Mtendaji wa gazeti hilo, Jacob Mugini, mjini Tarime jana Alhamisi.

Na Mwandishi Wetu
Tarime
--------------

Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Patrick Chandi Marwa, amelipongeza Gazeti la Sauti ya Mara kwa mchango wake mkubwa katika kutangaza mageuzi makubwa ya maendeleo yanayoendelea kushuhudiwa katika mkoa huo wa Kanda ya Ziwa.

Akizungumza jana Alhamisi mjini Tarime alipotembelea ofisi za gazeti hilo na kufanya mazungumzo na Mtendaji Mkuu (CEO) na Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Sauti ya Mara, Jacob Mugini, Chandi alisema chombo hicho cha habari kimekuwa mstari wa mbele kuibua na kuangazia mafanikio ya maendeleo ya sekta.

“Gazeti hili linasaidia sana kutangaza mageuzi makubwa ya maendeleo yanayoendelea kwenye mkoa wetu,” Chandi alisema na kuongeza kuwa Gazeti la Sauti ya Mara limeendelea kuripoti kwa weledi na hivyo kuwa daraja muhimu la kuwafikia wananchi kwa habari zenye kujenga na kuhamasisha maendeleo.

Mkoa wa Mara umebarikiwa kuwa na utajiri wa rasilimali asilia kama vile hifadhi bora Afrika - Hifadhi ya Taifa Serengeti, Ziwa Victoria, mifugo mingi na ardhi inayostawisha mazao mbalimbali, ikiwemo kahawa aina ya Arabica inayoendelea kusifika katika soko la dunia.

Kupitia rasilimali hizo na juhudi za wadau mbalimbali, mkoa huo unaendelea kushuhudia kasi kubwa ya maendeleo ya kisekta, huku vyombo vya habari kama Gazeti la Sauti ya Mara vikichukua nafasi yake kuweka wazi mafanikio hayo kwa jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages