
Ujumbe kutoka Liverpool FC Foundation ukikabidhi zawadi ya vifaa vya michezo kwa wanafunzi walioshiriki tamasha hilo wilayani Serengeti.
Serengeti
-----------------
Ujumbe kutoka Liverpool Football Club Foundation ya nchini Uingereza inayofadhili mradi wa ‘Save Her Seat’ umefika katika wilaya ya Serengeti na kujionea maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo.
.jpg)
Natasha akishiriki mchezo wa mpira wa miguu wakati wa tamasha hilo
Tamasha hilo la michezo lilifanyika Machi 5, 2026 kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Natta-Bigo iliyopo kata ya Natta wilayani Serengeti.
"Tunachofanya sisi (Liverpool FC Foundation) na Right to Play ni kuleta watu pamoja kupitia michezo ili kujifunza na kushiriki mapambano ya kuleta usawa wa kijamii, na kwa kweli tumefurahi sana kuwepo maeneo haya na tumeona watu wa jamii ya Natta ni wazuri na wakarimu sana," alisema Colin.
Naye Natasha alisema "Tumeona wanawake wengi wa Kiafrika wenye mafanikio makubwa kama wanasheria na wanamichezo pia, kwa hiyo kupitia hii michezo mabinti wadogo wanajenga umoja na kuhamasika kutokatia tamaa ndoto zao hata kama wanakumbana na mazingira magumu kiasi gani."

Natasha akizungumza katika tamasha hilo
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miradi kutoka AICT Dayosisi ya Mara na Ukerewe, Charles Mashauri, aliishukuru Liverpool FC Foundation kwa kufadhili mradi huo na kuiomba taasisi hiyo kuendelea kutoa msaada ili jamii iendelee kupata elimu zaidi.
"Tunawashukuru sana Liverpool FC Foundation kwa kutoa michango na kutuwezesha kuendeleza shughuli hii ya kutoa elimu kwa jamii juu ya vikwazo mbalimbali vinavyomzuia mtoto wa kike kupata elimu na tunaomba waendelee bila kuchoka," alisema Mashauri.
.jpg)
Mashauri akizungumza katika tamasha hilo
Akizungumza kwa niaba ya wanajamii wa Natta, Avelina Masota Mwengi, naye aliishukuru taasisi hiyo kwa kufadhili AICT na Right to Play ili kusaidia kuhamasisha jamii kuachana na mila kandamizi kwa watoto wa kike kama vile ukeketaji na ndoa za utotoni.
AICT na Right to Play zimekuwa zikishirikiana kutekeleza mradi wa Save Her Seat kwa ufadhili wa Liverpool FC Foundation kwa lengo la kusaidia watoto wa kike katika wilaya za Serengeti na Tarime, mkoani Mara kupata ujuzi utakaowasaidia kukabiliana na vikwazo vya kupata elimu.

Wasanii wa ngoma ya asili wakionesha umahiri wao katika tamasha hilo
Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara

No comments:
Post a Comment