NEWS

Sunday, 22 March 2026

Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi azindua Mfumo wa Kutabiri Kiasi cha Maji kwenye Mito



Makamu wa Rais Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi (wa pili kulia), wakati wa uzinduzi wa Mfumo wa Utabiri wa Kiasi cha Maji kwenye Mito, mkoani Morogoro, leo Machi 22, 2026.

Na Mwandishi Wetu
Morogoro
-------------------

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amezindua Mfumo wa Utabiri wa Kiasi cha Maji kwenye Mito nchini.

Uzinduzi huo umefanyika leo Machi 22, 2026 katika la Bwawa la Mindu Mjini Morogoro, ambako amejionea namna Wizara ya Maji inavyoshiriki katika utunzaji, ulinzi na uendelezaji wa rasilimali za maji.


Bwawa la Mindu Mjini Morogoro

Akizungumza katika hafla hiyo fupi, Mkurugenzi wa Bodi ya Maji Bonde la Wami Ruvu, Mhandisi Elibariki Mmasi, amesema mfumo huo ni moja ya jitihada za Wizara ya Maji za kuondoa changamoto za sekta ya maji kwa kuwezesha upatikanani wa taarifa sahihi za kiwango cha maji.

Mhandisi Mmasi amesema bwawa hilo ni sehemu ya maeneo yatakayonufaika kwani linapokea maji kutoka sehemu mbalimbali za nchi na linachangia kwa zaidi ya asilimia 70 ya huduma ya majisafi katika mji wa Morogoro.

Pamoja na uzinduzi wa mfumo huo, Makamu wa Rais Nchimbi amepanda miti rafiki wa maji kwenye chanzo hicho, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Maji Duniani na kilele cha Wiki ya Maji Tanzania.


Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi akimwagilia maji mti alioupanda jirani na Bwawa la Mindu Mjini Morogoro.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages