
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Dkt. Zabron Masatu (katikati), akipokea msaada wa vifaa tiba kutoka kwa Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa, CPA Rajabu Kinande, vitakavyosaidia kuboresha huduma za matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwl. Nyerere iliyopo Kwangwa, Musoma, jana.
Na Christopher Gamaina
Musoma
------------------

Musoma
------------------
Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere iliyopo Kwangwa, Musoma mkoani Mara, imepokea msaada wa vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 100 kutoka Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Meneja wa PSSSF Kanda ya Ziwa - anayehudumia mikoa ya Mwanza, Mara na Simiyu, CPA Rajabu Kinande, alikabidhi vifaa hivyo kwa Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Dkt. Zabron Masatu, katika hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo Machi 26, 2026.

CPA Kinande alisema vifaa hivyo vinalenga kuboresha huduma kwa wagonjwa, hususan akina mama na watoto katika hospitali hiyo ya kibingwa.
Alibainisha kuwa msaada huo ni mwendelezo wa utaratibu wa PSSSF wa kurejesha kwa jamii sehemu ya faida inayotokana na uwekezaji wake.


No comments:
Post a Comment