NEWS

Friday, 27 March 2026

Mwanamke wa kwanza atawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Duniani



Dame Sarah Mullally akitawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Kanisa Anglikana Duniani

Na Mwandishi Wetu

Dame Sarah Mullally, 63, amekuwa mwanamke wa kwanza nchini Uingereza kutawazwa kuwa Askofu Mkuu wa Cantetbury.

Mwanamana huyo, ambaye alikuwa Askofu na Muuguzi Mkuu wa Uingereza, amehudumu nafasi ya Askofu Mkuu wa 106 wa Canterbury tangu Januari 28, mwaka huu.

Kwa kutawazwa kwake kuwa Askofu Mkuu wa Canterbury, Sarah atakuwa ni kiongozi wa Kanisa la Uingereza na Dhehebu la Anglikana duniani kote.

"Utotoni kwangu sikufikiria hatima iliyokuwa mbele yangu," alisema Sarah baada ya kutawazwa.

"Nikitazama nyuma yangu kama kijana Sarah aliyemwamini Mungu na kudhamiria kumfuata Yesu, sikuwahi kufikiria hatima yangu mbeleni wala kushika nafasi hii niliyonayo," aliwambia watu 2,000 waliohudhutia sherehe ya kutawazwa kwake kwenye Kanisa la Canterbury.

Katika mahubiri yake ya kwanza kwa waumini wa Anglikana, Askofu Mkuu huyo mwanamama alionya kuhusu kile alichokiita "kusahauliwa kwa watu walioumizwa na udhaifu wa makanisa na jamii zetu."

Maaskofu Wakuu wote 105 wa Canterbury wamekuwa ni wanaume tangu Mtakatifu Augustino mwaka 597 baada ya kuzaliwa kwa Kristo.

Wanawake kwa mara ya kwanza waliruhusiwa kuwa wachungaji katika Kanisa Anglikana mwaka 1994.

Sherehe ya kutawazwa kwa Sarah - aliyeolewa na mwanamkakati wa teknohama, Eamonn Mullally, ilifanyika Jumatano Machi 25, 2026 na kushuhudiwa na waumini wa Kanisa Anglikana dunia nzima kupitia runinga.

Sherehe hiyo ilihudhuria na familia ya kifalme ya Uingereza.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages