NEWS

Friday, 6 March 2026

TAKUKURU yazindua ofisi yake mpya Bunda




Na Mwandishi Wetu
Bunda
---------------

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Crispin Chalamila, amezindua ofisi mpya ya taasisi hiyo katika wilaya ya Bunda, mkoani Mara.

Chalamila alizindua ofisi hiyo Machi 5, 2026 na kuipongeza TAKUKURU Wilaya ya Bunda kwa usimamizi mzuri wa mradi huo na matumizi sahihi ya fedha iliyotolewa na kubakiza shilingi million 31.

Aliishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uonmgozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa ofisi kadhaa za TAKUKURU ngazi za wilaya na mikoa nchini.

Aidha, Chalamila aliwataka watumishi wa TAKUKURU Wilaya ya Bunda kutunza miondombinu ya jengo la ofisi hiyo na kutoa huduma bora kwa wananchi.
Awali, Mkurugenzi wa Milki TAKUKURU, Emmanuel Kiabo, alisema fedha zilizotolewa kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo ni shilingi milioni 394.3, zilizotumika ni shilingi milioni 363.1 na kiasi kilichobaki ni shilingi milioni 31.1.

Kiabo alibainisha kuwa ujenzi wa ofisi hiyo umetekelezwa kwa mfumo wa ‘force account’.

Hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo ya TAKUKURU ilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Bunda, Aswege Kaminyoge, miongoni mwa viongozi wengine.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages